Tunayo stori kutokea kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri ambapo amefanya ziara katika Mradi wa Bomba la Mafuta unaoshirikisha Tanzania na Zambia (TAZAMA) kwa jailli ya kukagua miundombinu ya eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Sarah amesema mradi huo mkubwa umehusisha nchi mbili ukiwa wa kitaifa ambapo ulimkutanisha aliyekuwa rais wa Tanzania, Julius Nyerere na Rais Keneth Kaunda wa Zambia.
Amesema mradi huo unafanya kazi vizuri na unaendana na mabadiliko ya teknolojia kutokana na kubalidilishwa kwa baadhi ya vifaa ukiwa na Pampu ya kwanza ya mafuta kutoka Tanzania hadi Zambia.
“Kuna baadhi ya maeneo wananchi wanavamia ambapo Bomba limepita hivyo nikiwa kama Mkuu wa Wilaya kuna haja ya kuangali bomba lililopita kwani wananchi kukaa karibu na bomba hili ni hatari sana,“amesema.