Club ya Yanga SC imetangaza kuwa mchezaji wake Denis Nkane “The Wonder Kid” amepata majeraha na sasa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki 6, Taarifa hiyo imetolewa na Dr wa Yanga SC Moses kupitia Yanga SC App
“Winga wetu Deniss Nkane atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita baada ya vipimo kuonyesha amevunjika mfupa mdogo unaosababisha nyonga kujikunja, akitoa taarifa hiyo, daktari wa Yanga, Moses Etutu alisema Nkane atakuwa na vipindi viwili vya kuuguza majeraha yake hadi hapo atakaporejea rasmi uwanjani”
“Vipimo vimeonyesha alivunjika mfupa unaosababisha nyonga kukunja ndio maana alipata maumivu makali sana. Tayari tumeshaanza ratiba ya matibabu na atakuwa na vipindi viwili kabla ya kurejea moja kwa moja uwanjani, atakaa nje kwa wiki nne halafu wiki mbili za mwisho ataanza mazoezi mepesi ambayo tutakuwa tunamfuatilia tujue maendeleo yake,” DR Moses.