Habari za Mastaa

Huu ndio mwisho wa ndoa ya Mariah Carey na Nick Cannon

on

1

Nick Cannon na Mariah Carey walifunga ndoa mwaka 2008 na katika maisha yao wamefanikiwa kupata watoto wawili Monroe Cannon na Moroccan Scott Cannon. Story mpya hivi sasa kuhusu hawa wawili ni kwamba waliachana tangu mwezi wa tano mwaka huu.

Vyanzo mbalimbali vinaripoti kwamba sababu ya ndoa hii kuvunjika ni pale Nick Cannon alivyofanya mahojiano na Big boy wa Power 106 FM na kutaja wanawake ambao aliwai kujihusisha nao kwenye mapenzi. Kati ya wanawake aliowataja ni Kim Kardashian na wengine.

Inasemekana kitendo hicho hakikumfurahisha Mariah Carey ambaye alijiskia kuaibishwa kwa mume wake wa ndoa kuzungumzia hizo story kwenye radio kubwa ambayo watu wengi walikuwa wanasikiliza. Hivi sasa wawili hao wanafuatilia mambo ya kisheria kumaliza taratibu za kuvunja ndoa yao.

 

Tupia Comments