Habari za Mastaa

Maneno ya Nicki Minaj kuhusu Lil Wayne.. Maana ya tattoo zake je?

on

nicki miiiiii

Nicki Minaj ni msanii wa kike ambaye tunaweza kumuweka kwenye level moja na mastaa kama akina Beyonce, uwezo wake wa kudondosha hits umefanya awe mmoja kati ya wasanii wakubwa kwenye muziki Duniani.

Kwenye moja ya Interview moja aliwahi kufanya hiki ndio alichokijibu kuhusu Lil Wayne >>> Nasukumwa sana na watu wanaopenda kufanya kazi, watu ambao hawatafuti sababu au visingizio vya kutokufanya kazi… Lil Wayne namkubali sana upande wa nidhamu yake ya kazi…sijawahi kuona! Watu wakimwona Lil Wayne wanahisi vitu vingine lakini yule mtu yuko serious na sanaa yake na ni mmoja kati ya wanaume wanaonisukuma sana mimi kufanya kazi hata kabla ya kuwa chini ya Management ya Young Money“>>>

Nicki-minaj-tattoo-picture

Alipoulizwa juu ya tattoo yake kwenye mkono wake wa kulia Nicki alisema >>> Kwanza hii tattoo ina historia ndefu sana, nilichora nikiwa na miaka 16… Baba yangu alikasirika sana akataka kunifukuza nyumbani… Imeandikwa Kichina, inamaanisha God Is Always With You… Napenda kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu wangu na hii tattoo ni moja kati ya vitu vinavyonikumbusha kuwa niko hapa duniani kwa sababu gani“>>>

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments