Michezo

TFF imemkabidhi rasmi Etienne Ndairagije Taifa Stars

on

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF leo limetangaza rasmi kuwa kocha Etienne Ndairagije ndio kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

TFF imethibitisha kuwa imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha Etienne Ndairagije, ambaye awali alikuwa akikaimu nafasi ya ukocha mkuu baada ya kufukuzwa Emmanuel Amunike.

Maamuzi yamefikiwa baada ya TFF kuridhishwa na kiwango cha Etienne akiiongoza Taifa Stars katika michezo saba kama kaimu kocha mkuu na kushinda game 3, sare 3 na kupoteza mchezo mmoja, kabla ya hapo Ndairagije alikuwa kocha wa Azam FC.

Hata hivyo Etienne akidumu na timu hiyo kwa mechi saba amefikia malengo yote ikiwemo kuiwezesha kufuzu fainali za CHAN 2020 zitakazochezwa Cameroon pamoja na kufika hatua ya makundi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia 2022.

Soma na hizi

Tupia Comments