Top Stories

MAHAKAMANI: Mbunge John Heche ameachiwa kwa dhamana

on

Mbunge wa Tarime Vijiji, John Heche amesomewa mashtaka 3 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuunganishwa katika kesi inayowakabili viongozi 7 wa CHADEMA akiwemo mwenyekiti Freeman Mbowe.

Wakili wa serikali, Faraja Nchimbi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa wanaomba kumuunganisha Heche katika kesi inayowakabili wenzake ambapo yeye atakuwa mshtakiwa wa 8.

Hakimu Mashauri alikubali kumuunganisha, ambapo Wakili Nchimbi amedai Heche anakabiliwa na makosa matatu ikiwemo kufanya mkusanyiko ama maandamano yasiyokuwa halali.

Heche ameachiwa kwa masharti ya dhamana ya kuwa na Wadhamini wawili watakaosaini Bondi ya Shilingi Milioni 20 kila mmoja, pia awasili kituo cha Polisi Central kila Ijumaa. Kesi imeahirishwa hadi April 16, 2018.

Mbunge CHADEMA, John Heche jinsi alivyofikishwa Mahakamani

Soma na hizi

Tupia Comments