Michezo

Picha za jinsi mpenzi wa yule bilionea mbaguzi wa Marekani anavyokwepa waandishi

on

Screen Shot 2014-05-06 at 4.17.32 PMHuyu mrembo anaitwa V Stiviano ambae ndio alivujisha maongezi ya simu kati yake na bilionea Donald Sterling ambae alitoa maneno mazito yenye ubaguzi dhidi ya watu weusi kwa kusema hataki kuwaona watu hao wakihudhuria kwenye mechi za timu ya basketball anayoimiliki iitwayo L.A Clippers.

Toka hii ishu imevuja Stiviano ambae alikua ni ‘nyumba ndogo’ ya Donald amekua akikwepa waandishi wa habari ambapo aliamua kuvaa kifaa maalum kabisa ili kuepuka kuhojiwa na waandishi wa habari.

Mmoja kati ya Wamarekani waliotoa maoni yao kuhusu Stiviano alisema ‘huyu binti anaweza kuwa mpuuzi wa kupindukia… japokua mimi ni Mweusi, sijali kama Donald alikua mbaguzi ama la… msichana kama huyu anawezaje kumsaliti mtu aliempa magari ya kifahari Ferarri, Bentley mbili na nyumba ya kifahari? huyu binti hajatenda haki’
Screen Shot 2014-05-05 at 1.25.55 PM

Bilionea wa kimarekani Donald Sterling alikiri kwamba sauti iliyosikika ikitoa maneno ya kibaguzi ni yake hivyo akaadhibiwa kwa kutojihusisha na timu yake milele na kulazimishwa kuiuza timu hiyo.

Screen Shot 2014-05-05 at 1.26.24 PM

Screen Shot 2014-05-05 at 1.25.42 PM

Screen Shot 2014-05-05 at 1.25.20 PM

Screen Shot 2014-05-05 at 1.25.06 PM

Screen Shot 2014-05-05 at 1.24.40 PM

V Stiviano na Donald

V Stiviano na Donald

Unapenda stori kama hizi zisikupite? nitakua nakutumia twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la @millardayo

Tupia Comments