Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.
Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya November 01 2016 ni hii kutoka gazeti la Tanzania daima yenye kichwa cha habari ‘Serikali yahakiki vyeti vya ndoa’
#TanzaniaDAIMA Serikali yahakiki vyeti vya ndoa kwa watumishi wake madai wamekuwa wakidanganya ili kupata nauli na stahiki zingine za likizo pic.twitter.com/HW06vcsywP
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
Gazeti la Tanzania Daima lemieripoti kuwa Serikali imeanza uhakiki wa vyeti vya ndoa kwa watumishi wa umma. Hatua hiyo ambayo imewashtua watumishi wengi wa umma, imeelezwa kuwa ni mwendelezo wa harakati za Serikali ya Rais John Magufuli kuhakiki watumishi wa umma ili kuondokana na watumishi hewa.
Wakati Serikali ikianza na uhakiki wa vyeti vya ndoa, kazi ya uhakiki wa watumishi hewa na vyeti vyao vya elimu inaendelea sehemu mbalimbali nchini.
Kwa muhibu wa Gazeti la Tanzania Daima habari ambazo limezipata zinasema kuwa serikali imeanzisha uhakiki huo nchi nzima kwa madai kuwa baadhi ya watumishi wa umma wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwamba wana ndoa ili kupata nauli na stahiki zingine za likizo wakati hawana ndoa.
Habari zaidi zinasema kuwa walimu wakuu wa shule zote za Wilaya ya Ilala wamepewa siku mbili kutekeleza agizo hilo kwa walimu wao. Mmoja wa walimu hao ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe, alilithibitishia Tanzania daima kuwa ametoa siku mbili kwa walimu wa shule yake wenye vyeti vya ndoa waviwasilishe kwake.
>>>’Kweli tumepewa agizo hilo leo manispaa ya Ilala na tumetakiwa kuwasilisha vyeti hivyo kesho na tayari baadhi ya walimu wangu wamefanya hivyo leo na kesho zoezi hilo linakamilika‘
Alipoulizwa sababu ya kuwepo kwa zoezi hilo, mwalimu huyo alisema hajui lakini anahisi lina lengo la kudhibiti taarifa za uongo za watumishi wakati wa kuomba likizo.
Wakati walimu wa shule za Ilala wakitakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ndoa, wilaya nyingine za Temeke, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni hawana taarifa hizo.
Mmoja wa walimu kutoka Manispaa ya Ilala alisema kuwa uhakiki huo una lengo la kutaka kuchelewesha zaidi malipo na stahiki za walimu za likizo ambazo hazijalipwa kwa miaka mingi.
Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya Tanzania leo November 1 2016
#MWANANCHI Raia wa China wametapeliwa mil 22.8 wakidai kuwa sauti waliyoisikia kwenye simu iliyotumiwa na tapeli ilifanana na ya RC Makonda pic.twitter.com/EP1cI7uHtf
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI Wabunge CCM, CHADEMA kwa nyakati tofauti wajifungia na viongozi kupanga mikakati dhidi ya hoja zitakazowasilishwa bungeni pic.twitter.com/X95I4hAkAd
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI Baadhi ya wazazi wa wanafunzi waliokosa mikopo ya elimu ya juu wameeleza kuwa hali zao kiuchumi sio nzuri pic.twitter.com/JqydxtnLlD
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI Baadhi ya wazazi wa wanafunzi waliokosa mikopo ya elimu ya juu wameeleza kuwa hali zao kiuchumi sio nzuri pic.twitter.com/JqydxtnLlD
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI Rais Magufuli afungua ukurasa mpya na kukoleza ushirikiano na Kenya, asema Kenya ni mshirika nambari moja kwa uwekezaji Tanzania pic.twitter.com/9t31q1SrFa
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI Upelelezi kesi ya kumtishia bastola trafiki inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mkinga, Mkumbo umekamilika, 18 kutoa ushahidi pic.twitter.com/f9AEABbJah
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#MWANANCHI DC Ilala, Sophia Mjema amesema leo watafanya operesheni ya kuwaondoa wamachinga kando ya barabara za mabasi yaendayo haraka pic.twitter.com/upnQDwQXon
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#NIPASHE JPM aweka wazi kuwa ana uhusiano mzuri na Rais wa Kenya na kufichua siri kuwa wamekuwa na mawasiliano ya simu mara kwa mara pic.twitter.com/6N9j40iMHv
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#NIPASHE Wabunge hatarini kukosa malazi Dodoma, baada ya wamiliki 73 wa nyumba za kulala wageni kugoma wakipinga tozo kubwa za manispaa pic.twitter.com/njrXH5n6g4
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#NIPASHE Bodi ya mikopo elimu ya juu imetangaza siku 90 kwa waombaji mikopo mwaka 2016/2017 kukata rufaa ikiwa hawakuridhishwa na upangaji pic.twitter.com/Z8xKf0yZBr
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#NIPASHE Machinga Mwanza wamegoma kuhamia maeneo yaliyotengwa kwa madai baadhi yana migogoro na mengine si mazingira rafiki kwa biashara zao pic.twitter.com/MbnLTKmQij
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#MTANZANIA Jukwaa la wahariri lamshutumu Mwenyekiti wa kamati, Serukamba kuwa kikwazo ktk kufanikisha Muswada wa sheria ya huduma za habari pic.twitter.com/aYtL7HSx9k
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#MTANZANIA Raia watatu wa China wamepandishwa kizimbani Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka mawili likiwamo la kumteka mwenzao pic.twitter.com/HCqpluGPtI
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#TanzaniaDAIMA Jeshi la zimamoto DSM limejikuta ktk mazingira magumu ya kutekeleza majukumu yake kutokana na uhaba wa vitendea kazi pic.twitter.com/gRWvdvo4on
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#TanzaniaDAIMA CWT Misungwi yatangaza maandamano ya amani kushinikiza mkurugenzi, Mwaiteleke aliyewadekisha walimu aondolewe ktk nafasi yake pic.twitter.com/tDYCC1xLoq
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
#MTANZANIA Rais Kenyatta akwepa kuzungumzia kashfa ya ufisadi wa bil 51 ktk wizara ya afya ambako baadhi ya jamaa zake wametajwa kuhusika pic.twitter.com/p6xeorYH6y
— millardayo (@millardayo) November 1, 2016
UMEKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV NOVEMBER 1 2016? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI