AyoTV

Walioghushi saini ya Waziri Makamba, wapewa masharti saba na mahakama

on

Leo November 14, 2018 tunayo story kutokea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Wafanyakazi watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamefanikiwa kupata dhamana baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi kuridhia kuwapatia dhamana.

Hatua hiyo inatokana na washtakiwa kupitia mawakili wao kupeleka maombi ya dhamana Mahakama Kuu kwa sababu washtakiwa hao wameshtakiwa chini ya sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo kesi hizo zinasikilizwa Mahakama Kuu.

Washtakiwa waliopata dhamana ni Ofisa wa Mazingira NEMC, Deusdith Katwale(38) na Mtaalam wa IT NEMC, Luciana Lawi(33) wote wakazi wa ubungo Msewe, Katibu Muhasi wa NEMC (Sekretari), Edna Lutanjuka (51) Mkazi wa Mbezi Beach St Gasper, Msaidizi wa ofisa Mwaruka Mwaruka (42) na Ofisa mazingira Nemc, Lilian Laizer (27) wote wakazi wa Ukonga Mombasa.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi ikiwamo la kughushi saini ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa Mazingira.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando amewasomea masharti ya dhamana washtakiwa hao ambapo kila mshtakiwa anatakiwa kuweka fedha benki kiasi cha Sh. Milioni 13.3 au kuwasilisha mahakamani hapo hati ya mali isiyoamisha yenye thamani ya fedha hiyo.

Pia kila mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, mmoja wapo awe mwajiliwa wa serikali, wenye vitambulisho vya Taifa watakaosaini bodi ya Sh. Milioni 2.5. Aidha, washtakiwa hao wametakiwa kutotoka nje ya Dar es Salaam pamoja na kuwasilisha hati zao za kusafiria mahakamani hapo.

Washtakiwa hao pia wametakiwa kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kama watakavyopangiwa.Kesi hiyo imeahirishwa hadi November 28, 2018 kwa ajili ya kutajwa.

A-Z: MZEE ALIYEKWENDA NA KIPANDE CHA GAZETI HOSPITALI YA MUHIMBILI ILI ATIBIWE HARAKA

Soma na hizi

Tupia Comments