on air with millardayo

Nisha kuhusu kazi maisha na mapenzi ‘sishtukagi na headlines, sijawahi kuwa na urafiki na Baraka’

on

Jina la kuzaliwa ni Salma Jabu ila umaarufu anao kupitia jina la Nisha akiwa ni miongoni mwa waigizaji hodari wa kike Tanzania, amekaa kwenye Exclusive na Millard Ayo kwenye OnAIRwithMillardAyo ambako ameongea ishu zake mbalimbali za maisha, kazi na mapenzi.

Kuna ripoti ziliandikwa kwamba ulikanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji Baraka Da Prince na ukasema humjui kabisa? JIBU >>>Sijawahi kuandika hicho kitu na huwa simuandiki mtu kwenye page yangu, sipendi kuhusisha maisha yangu binafsi na maswala ya kazi yangu kwenye mitandao, sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi, wa kirafiki au wa aina yoyote na Baraka Da Prince’

Umeshawahi kuwazia chochote kuhusu spidi ndogo ya Bongo movie kwenda nje ya mipaka ya Tanzania?

JIBU >>> ‘Mimi na timu yangu tulikaa tukalitazama hilo pia kama unakumbuka miezi miwili iliyopita kuna picha ziliruka nikiwa na mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi, kuna kitu kikubwa kinakuja kitahusisha soko la Afrika Mashariki

Sasa hivi una umri wa miaka 27, una mtoto tayari?

JIBU >>>Ninae mtoto wa kike ana umri wa miaka 11, nilimpata nikiwa na miaka 17…. mitihani ya kidunia inatokea kila mtu ana historia yake, nilijutia lakini unaizoea ile hali na kujifunza kupitia ulipokosea…  ni stori ya kusikitisha na nikiiongea itaniumiza nitaanza kulia lakini ni kitu kiliniathiri sana kisaikolojia’

Ukitaka kujua mengi zaidi ya Nisha unaweza kutazama hii video hapa chini…

ULIIKOSA YA WASTARA ALICHOSEMA KWANINI NDOA YAKE IMEVUNJIKA NDANI YA SIKU 80? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE 

Soma na hizi

Tupia Comments