Mkali wa miondoko ya RnB Chris Brown ametoa ahadi ya kuileta ngoma ya pamoja na rapper Drake hii ni baada ya wawili hao kuonekana wakiwa na utofauti wa muda mrefu na kuripotiwa kuwa chanzo cha bifu kati yao ni mwanadada Rihanna.
Chris Brown aliwahi pia kuongea kuhusu kolabo hiyo na Drake usiku wa sherehe ya birthday yake May 5,2019 na wengi hawakuamini ujio wa ngoma hiyo, sasa kupitia ukurasa wa instagram yake amethibitisha hilo na kuandika ‘msimu huu wa joto naona kama joto litaongezeka”
Mpaka sasa wawili hao hawajawahi kuongea kuhusu tofauti zao ingawa Chris Brown aliwahi kuwa mapenzini na Rihanna na baadae kuachana ukaribu wa Drake na Rihanna ulileta maswali mengi na wengi kudai kuwa wawili hao walikuwa wanamahusiano ya kimapenzi pia kitu ambacho kilidaiwa kutomfurahisha Chris Brown.
VIDEO: NOMA!! NANDY NA WILLY PAUL WALIVYO PEWA SHANGWE SUMBAWANGA