Habari za Mastaa

Case closed! Rapper Young Thug afutiwa shtaka la kumiliki silaha

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa rapper Young Thug amefutiwa shtaka la kukutwa na silaha mwezi August 2018 ambapo alikamatwa kwa kosa hilo, leo June 19,2019 imeripotiwa kuwa umekosekana ushahidi wa kutosha kuthibitisha kosa hilo.

Mwanasheria wa Young ThugMichael Goldstein ameikataa kesi na kusema kuwa shauri hilo limefutwa kwa kukosekana kwa ushahidi wa kutosha ambapo inadaiwa kuwa silaha iliyokutwa ndani ya gari alilokuwa akilitumia Young Thug polisi wameshindwa kubaini DNA ya muhusika ikiwa gari hilo lilikuwa na jumla ya watu watatu hivyo kesi hiyo imefutwa.

Young Thug alikamatwa wakati wa sherehe ya kusikiliza album yake “Slime Language” mjini Los Angeles mwezi August,2018 ambapo Polisi walimkamata lakini mmoja kati ya rafiki wa YT alikimbia ndani ya gari la Polisi ndipo polisi waliposhtuka na kufanya uchunguzi kwenye gari la YT na kukuta silaha.

VIDEO: UMEPITWA NA HII YA SIKU 7 ZA WEMA GEREZANI ZAMTESA AUNT EZEKIEL? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments