Ni July 3, 2024 ambapo Bodi ya Mikopo Heslb inafanya mahojiano na Clouds TV katika kipindi cha Sentro kuhusu kampeni mpya ya Fichua Maalumu inayolenga kuwashirikisha wananchi kwa kutumia simu na mitandao ya kijamii, kuwafichua wadaiwa sugu wa mikopo ya elimu ya juu.
“Kwenye kampeni hii tunafanikiwa lakini katika mafanikio kuna changamoto. Na changamoto kubwa na imekuwa ni ya kawaida kwenye hii biashara ya kukopesha na kudai. Kuna watu tabia yao ni kukwepa kulipa madeni”- George mziray, Mkurugenzi wa Urudishaji Mikopo
“Na kumekuwa na tafsiri ambayo sio sahihi kati ya mtu mwenye kipato na mtu aliyeajiriwa. Utakuta mtu amenufaika na anafanya biashara anapata kipato cha kila siku lakini ukimwambia arejeshe mkopo anakwambia hajaajiriwa. Hajapata ajira” George mziray, Mkurugenzi wa Urudishaji Mikopo
“Na tumekuwa tukitoa elimu kuwaambia kwamba kinachotakiwa hasa ni kipato awe ameajiriwa au hajaajiriwa, amejiajiri mwenyewe anatakiwa kulipa deni la mkopo wa vyuo vikuu”- George mziray, Mkurugenzi wa Urudishaji Mikopo