Hapa nimekusogezea Nukuu za jerry Silaa Mbunge wa Ukonga akizungumzia kuhusu Uwekezaji wa bandari.
“Mkataba ulioingiwa una lengo moja tu, linatajwa kwenye ibara ya 2(1) ambalo ni kutengeneza msingi wa kisheria wa ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Falme ya Dubai kwenye maeneo ya uwekezaji wa bandari.”- Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa
“Maoni ya wananchi bado yanapokelewa, kwa sababu ipo mikataba mingine. Unapoleta andiko utasema gharama zako za uwekezaji ni kiasi gani, unaleta wataalamu wangapi, muda wa kurejesha mradi wako ni muda gani na mwisho ndiyo utapata muda wa mradi utakuwa miaka mingapi.“- Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa
“Kwenye uwekezaji ama uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam; ibara 5 inataja mambo matatu, atafanya uendelezaji, usimamizi ama uendeshaji. Kazi anayoenda kuifanya ni kupakia na kupakua mizigo na kuhudumia shehena ya mizigo; masuala yote ya kodi yatafanywa na TRA.”- Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa
“Niwathibitishie, ibara 22 inatoa fursa ya marekebisho kufanyika kwenye mkataba huu. Maoni yote tuliyopokea kwenye kamati ya Bunge mengi yalijikita kwenye mikataba miwili na yote tumewasilisha Serikalini”- Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa
“Wengi wanasema kuwa, kila fursa ya uwekezaji wa bandari lazima mwekezaji wa Dubai apewe yeye, sio kweli. “Ibara ya 4(2) inasema kwamba, itakapotokea fursa Tanzania itawataarifu wawekezaji hawa (DP World) ili waweze kuleta maandiko yaweze kufikiriwa, ili kama yataafikiwa waweze kuingia kwenye shughuli za uwekezaji”- Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa