Mfumo wa afya wa Lebanon unajitahidi kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ys afya huku kukiwa na mashambulizi yanayoendelea Israel, mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema.
“Kati ya vituo 207 vya huduma za afya za msingi katika maeneo yenye migogoro nchini Lebanon, 100 sasa vimefungwa kutokana na kuongezeka kwa ghasia. Hospitali 5 zimefungwa kwa sababu ya uharibifu wa miundo kufuatia mashambulizi,” Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema kwenye X Jumamosi.
“Mashambulizi dhidi ya wafanyikazi wa afya na vituo, ambayo yamesababisha karibu vifo 100, lazima yakome,” alihimiza.
Akibainisha kuwa idadi ya watu waliojeruhiwa inaongezeka, mkuu huyo wa WHO alisema mfumo wa afya unatatizika kuhimili kutokana na uwezo mdogo wa watu na rasilimali.
Ghebreyesus alitoa wito wa ulinzi wa haraka wa wagonjwa, na wafanyikazi wa afya.