Nyumba/ Mijumba

Nyumba nzuri sio mamilioni… ni mipango na utundu kidogo kama hivi !!

on

n1Ni mara ngapi unatembelea nyumba ya mtu mwenye pesa zake alafu unagundua kazidisha vitu mpaka nyumba haina mvuto tena? sasa kupitia millardayo.com nitaendeleza utamaduni wa kuziweka picha za nyumba za kisasa zilizojengwa kwa gharama ndogo lakini zinavutia.

n2Ukitazama kwenye picha ya kwanza na ya pili utaona jinsi sebule ilivyo na vitu vichache lakini inavutia, picha zimewekwa kwenye ukuta mmoja tu na kamaliza kazi ya picha, kochi moja la kona na meza ndogo ya kuvutia.

n3Siku hizi vitu vingi sana vinapatikana Tanzania kwenye maduka mbalimbali…. mfano kinachoonekana hapa ni sakafu ya mbao pia ambapo Tanzania nimeiona na nyingine nyingi za aina hiyohiyo ya mbao ambazo haziitaji kudekiwa, ni kufuta na kitambaa chenye unyevunyevu, kamalizia na ukuta mzuri ulioonyooka na kupakwa rangi.

n4

n5Hapa ni jikoni na mpaka panakuvutia kupatazama kila time, vitu ni vichache na rangi iliyopakwa inaendana na eneo lenyewe…

n6

n7

n8

n9

n10Kwa wale Mabachela au wenye familia zao bado sebule kama hii ni nzuri kwao… ukuta umetengenezwa vizuri kwa matofali ya kuchoma alafu yakapakwa rangi nyeupe, mpangilio wa taa pia ambazo zinapatikana Tanzania ukamalizia uumbaji wa hii sebule nzuri.

n11Kwenye jiji kama la Dar es salaam, Mwanza au Arusha watu ni wengi town na unaweza kuwa na eneo dogo tu la nyumba lakini ukalitumia vizuri kwa kupangilia ndani, mwishowe ndio inakua kama hivyo sebule na dining ndogo tu.

n12Wakati mwingine kuifanya nyumba ivutie zaidi unaweza kuepuka kuweka wallpaper zenye michoro au vitu vingi, huu ukuta mweusi kwenye picha za juu na hii hapa chini unadhihirisha hilo… simple lakini poa sana.

n13Ubunifu wa kutengeneza kitanda kama hicho kwa mbao hata bongo kuna mafundi wazuri tena sana wa kufanya hivi, hizo taa madukani zimejaa na unaweza kuzipata kwa kati ya elfu 70 mpaka laki moja.

n14Kwa leo ni hayo tu nilikua nayo mtu wangu… kama una chochote nitafurahi ukiniachia kwenye comment hapa chini…

n15

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments