Utafiti mpya uliyofanywa na Chuo Kikuu cha New York, Marekani umegundua mnyama mwingine ambaye ana ubongo mkubwa sawa na binadamu ambapo utafiti huo ulionesha jinsi gani mazingira wanayoishi binadamu na Nyani yanavyoshabihiana na kuwafanya kuwa wanyama pekee wenye ubongo ulio sawa kwa ukubwa.
Mkuu wa utafiti huo Alex Decasian alizungumza na BBC >>> “Nyani hasa jamii ya Orangutans wana ubongo ulio sawa na binadamu kwa kuwa hupitia changamoto zinazofanana, nyani mwenye umri mkubwa ana ubongo mkubwa zaidi kuliko Nyani mtoto, hii inasadia katika ulinzi wa jamii yao na kutatua matatizo kama ugomvi”
Utafiti huo pia ulionesha nyani anayekula matunda ana ubongo mkubwa zaidi ukilinganisha na nyani anayekula majani na mizizi ambapo Mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford amesema ubongo mkubwa humtofautisha nyani na wanyama wengine katika uelewa wa mambo, kuwa na huruma na kutambua majukumu yao.
VIDEO: Ilikupita ya Tembo mtoto anayekunywa maziwa ya Tsh 200,000 kwa siku? Bonyeza play kutazama hapa chini.
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo