Habari za Mastaa

Chris Brown adaiwa kumlaani Mtoto, Mama apiga Biblia ukutani

on

Inaripotiwa kuwa usiku wa Jumamosi May 4,2019 mwimbaji  Chris Brown alipata ugeni nyumbani kwake Tarzana California na mwanamke mmoja toka mjini Texas ambaye alikuja na mwanae wa kiume akidai kuwa Chris Brown aliwahi kumlaani. 

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ unaripoti kuwa ilibidi walinzi waripoti tukio hilo polisi na baada ya muda mchache walifika na kumkuta mwanamke huyo akishika Biblia na kuirusha kwenye ukuta wa nyumba ya staa huyo wa R&B, baada ya polisi kuhoji mwanamke huyo alisema kuwa amefika hapo kuondoa laana aliyopewa mwanae na Chris Brown hivyo kwa kuitundika Biblia ukutani itasaidia kuifuta laana hiyo.

Polisi walihitimisha kwa kusema mama huyo hayupo vizuri kiakili (mentally unstable) na alichukuliwa kwa ajili ya tathmini na mwanae alipelekwa rumande. Wakati tukio hilo linatokea Chris Brown hakuwepo ndani, alikwenda kwenye birthday party ya rapper Desiigner.

VIDEO: HILI NDILO JUMBA LA KIFAHARI LA REGINALD MENGI MACHAME, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA 

Soma na hizi

Tupia Comments