Breaking News

BREAKING: Nyalandu kuhusu alichozungumza na Lowassa leo

on

Kama unakumbuka siku za hivi karibuni aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu alitangaz0 kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwemo Ubunge wa Singida Kaskazini na kutangaza kuwa atahamia CHADEMA.

Sasa leo November 7, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake, Mikocheni Dar es Salaam na akaandika haya kupitia twitter yake…

>>>MAPEMA leo, nimekutana na kufanya mazungumzo na Edward Lowassa ofisini kwake, Mikocheni, mjini Dar es Salaam kuhusu UMUHIMU wa kuimarisha UMOJA miongoni VYAMA vya UPINZANI nchini Tanzania tukiwa tunaelekea Uchaguzi Mkuu 2020. IMEANDIKWA: Wazee WATAWALAO vyema, wanastahili HESHIMA maradufu. Asante sana #EdwardLowassa!

ULIKOSA? Lazaro Nyalandu akitangaza kujiuzulu Ubunge na nafasi zote CCM, Bonyeza play hapa chini kuitazama

Soma na hizi

Tupia Comments