Hii ni sehemu nyingine inayowakutanisha watu wengi kwa sasa, yani ni kitu kipya ambacho kimepata mapokezi makubwa ndani ya muda mfupi tena kwenye mikoa mbalimbali Tanzanai Dar es salaam ikiwemo.
Upande wa burudani SkyLight Band ndio ilikua miliki yao lakini pia kulikua na MaDJ wakali kuukamilisha huu usiku vizuri akiwemo Dj Summer na mtangazaji Adam Mchomvu.
Usiku huu pia ndio washindi wawili walijulikana ambao watasafiri na mtu wako wa nguvu Millard Ayo kwenda Amsterdam Uholanzi kwa ajili ya kula hizo good times kila kitu kikiwa ni VIP kwa usimamizi wa Heineken.
Wa kwanza ni Caroline kutoka Heineken, na hawa wa katikati ndio washindi nitakaokwenda nao Amsterdam kuenjoy.
Umeshawahi kupata nafasi ya kuenjoy kwenye hii Nyamachoma?