Top Stories

Nyanshiski afunga ndoa, sherehe ya siri

on

Mwanamuziki Nyamari Ongegu maarufu Nyanshiski amefunga ndoa na mpenzi wake Zia Bett katika hafla ya faragha iliyofanyika mapema Desemba 10, 2021.

Nyota huyo alisindikizwa na mastaa kadhaa akiwamo aliyekuwa mshirika wake mkubwa kwenye bendi yake ya Kleptomaniax, Dj Stylez, Big Pin, pamoja na Wahu.

Huku nafasi ya mpambe wake ikishikiliwa na meneja wake wa zamani ambaye kwa sasa ni mtayarishaji wa Filamu maarufu nchini humo Fakii Liwali pamoja na msanii Nameless. Nyashiski na Zia Bett ni wapenzi wa muda mrefu na wamebarikiwa kupata mtoto mmoja.

“C.E.O BARBARA AMEFANYA VURUGU LEO AKIINGIA VVIP, WALIKUJA NA TICKET ZA WATU WENGINE” – TFF

Soma na hizi

Tupia Comments