Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif amesema Walimu waliielewa vizuri kauli ya Rais Samia Suluhu aliyoitoa kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi kuhusu ahadi ya nyongeza ya mishahara ambapo wamemshukuru kwa kuitimiza ahadi hiyo na kuridhia nyongeza ya 23.3% ya mishahara kwa Watumishi.
“Baada ya kauli yako ya Mei Mosi, Mh. Rais, Walimu tulikuelewa na tukasema tupo pamoja nawe, tunachapa kazi, kama uliweza kuwapandisha madaraja (vyeo) katika katika kipindi cha mwaka 2021/2022 pekee 92.9% ya Walimu wote ambao ni takribani 260,000, hata hili la kuongeza mishahara tulijua tu litafanikiwa”“Kama umetoa ajira kwa awamu nne, ya kwanza Walimu 13,000, ya pili 7000, ya tatu 6000 na ya nne ni hii ya juzi 12,000 ambayo ni sawa na 15% ya Walimu waliopo na kupandisha Madaraja (Vyeo) Mwaka jana Walimu 127,000 na mwaka huu zajdi ya 60,000, watakaonufaika na Daraja la Mserereko ni Walimu 52,0000 ambapo jumla ya walionufaika ma Madaraja ni sawa na 92.9%, hata hili la mishahara tulijua litakamilika tu”