Michezo

Kiungo alieinyanyasa Taifa Stars atua rasmi Simba SC

on

Kutoka ndani ya Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba leo July 4, 2019 tunayo taarifa ya kusajiliwa kwa kiungo wa Timu ya Taifa ya Kenya pamoja na Klabu ya Gor Mahia Francis Kahata.

Simba SC wameandika katika page yao ya Instagram “Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheza eneo la kiungo, kwasasa akiwa sehemu ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya kilichoshiriki AFCON 2019”

“Francis Kahata (27) msimu ujao atavaa jezi ya Mabingwa wa nchi baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili”

Kahata amejiunga Msimbazi akitokea Gor Mahia ya Kenya ambapo akiwa kwenye klabu hiyo alishinda Kombe la Ligi Kuu mara tatu, kiungo bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Kenya mara mbili na mchezaji bora wa msimu 2018/2019 wa Gor Mahia.

KINACHOMFANYA BONGOZOZO ASITE KUOMBA URAIA TZ, MAISHA YAKE?

Soma na hizi

Tupia Comments