Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo leo Agosti 23, 2021 amezungumza kupitia kipindi cha Clouds360 kinachorushwa Clouds TV kuhusu mfumo mpya wa ulipaji wa kodi ya Majengo.
“Naomba niweke wazi Wananchi wasiwe na taharuki nyumba za Vijijini haziko katika mpango wa kutozwa kodi ya majengo vilevile nyumba zilizojengwa kwa vifaa ambavyo sio vya kudumu kama zile udongo zilizoezekwa kwa nyasi hazihusiki na kodi ya majengo”-Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA
“Kodi ya majengo ni kodi ambayo inatozwa kutokana na maendelezo juu ya ardhi, mara nyingi Watu wanaichanganya na kodi ya ardhi, hii kodi ya ardhi inalipwa kule Wizara ya ardhi kodi ya pango la ardhi ni ardhi ambayo haina chochote au ina jengo juu yake, kodi ya jengo ni yale maendelezo juu ya ardhi ndio inayolipwa kwa sasa”- Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA
“Na kodi hii mwanzoni ilikuwa ikikusanywa na wenzetu wa Local Government na baadae ikahamishiwa TRA na wakati tunaanza kuikusanya utaratibu ulikuwa tofauti kidogo ilikuwa jengo linathaminishwa alafu inatozwa kwa asilimia fulani ya hiyo thamani ya jengo”- Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA
“Kiukweli utaratibu huu ulikuwa na usumbufu sana utakuta nyumba zilizothaminishwa zinakuwa ni chache ukilinganisha ambazo hazijathaminishwa, utakuta mtaa mwingine nyumba yake imethaminishwa analipa asilimia na mwingine nyumba yake haijathaminishwa analipa Tsh. Elfu 10 “——— asema Mkurugenzi wa Huduma na Elimu Kwa Mlipa kodi Richard Kayombo kwenye Clouds360 ya Clouds TV
“TUNAKUSHAURI UNUNUE UMEME WA ELFU 2000 ILI UWEZE KULIPA KODI YA MAJENGO”- TANESCO