Ni sehemu kubwa ya vitu ninavyovipenda duniani, nyumba nzuri huwa zinanivutia sana na sisiti kuhifadhi hata picha ninazokutana nazo kila siku.
Leo nimepata hizi nikasema niwawekee watu wangu hapa, najua kuna ambao wanajenga, kuna ambao wameshajenga tayari lakini wanaweza kurekebisha na kuna ambao hawajajenga ambao uzuri wa nyumba kama hizi unaweza kuwapa nguvu zaidi ya kupambana na maisha au kuwapa idea kwenye kile kidogo walichonacho.
Hata kama hutojenga au hauna uwezo wa kuwa na nyumba kama hii, imani yangu ni kwamba ukitazama hizi picha unaweza kuokota chochote kama idea na ukaihamishia kwako.
Hii nyumba ya juu ipo Dorset England.
Hii nyumba inayofata hapa chini ipo Texas Marekani.
Sometimes huwa tunasumbuka kuweka taa kwenye nyumba zetu au tunaweka taa ambazo labda hazivutii kuwekwa kwenye nyumba ila picha kama hizi zinatufundisha vitu vingi sana ikiwemo taa za nje ya nyumba, taa inapomulika ukuta kama hivyo mwanga unapatikana na ukiwa na mvuto pia.
Umependa nini au umeipenda zaidi nyumba gani kwenye hii post ya leo mtu wangu? nitafurahi kusikia kutoka kwako ili inipe nguvu zaidi pia ya kupost picha za nyumba kila wakati hapa millardayo.com
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook