Baada ya kusota mahabusu kwa takribani miaka 4, Hatimaye aliyekuwa Mkurugenzi wa IPTL, mfanyabiashara James Rugemalira ameachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi. Rugemalira alifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 19, 2017 pamoja na wenzake wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2027 yenye mashtaka 12.
Mashtaka ya Rugemalira yameondolewa chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwanendo wa Makosa ya Jinai, DDP amefuta mashtaka hayo na yeye kuachiwa huru. Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili wanadaiwa kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19,2014 jijini Dar es Salaam, walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India kwa ajili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
TAZAMA VIDEO RUGEMALIRA ALIVYOFIKA KANISANI BAADA YA KUACHIWA HURU