Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayekipiga katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta, msimu huu ameonekana kudhamiria zaidi kufanya makubwa katika timu yake kutokana na kuisaidia kupata matokeo katika game muhimu kwa timu hiyo.
Samatta kama kawaida usiku wa January 18 alikuwa sehemu ya kikosi cha KRC Genk kilichocheza mchezo wa Derby ugenini dhidi ya Sinti Truiden na kufanikiwa kupata matokeo ya ushindi wa magoli 3-2 licha ya kutanguliwa mara mbili, magoli ya KRC Genk yalifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 28 na akatoa assist ya goli dakika ya 75 kwa Trossard kabla ya Ndongala kufunga goli la ushindi dakika ya 80.
Magoli ya Sinti Truiden yalifungwa dakika ya 2 na Botaka na Boli dakika ya 70, ushindi huo sasa umeifanya KRC Genk iongoze Ligi kwa kuwa na jumla ya pont 51 wakifuatiwa na Club Brugge waliopo nafasi ya pili wakiwa na point 41, Samatta kwa upande wake leo amefunga goli lake la 16 la Ligi Kuu Ubelgiji msimu huu na kuendelea kuwa kinara wa ufungaji msimu huu akifuatiwa na Landry Dimata wa Anderletch akiwa na magoli 13.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”