Michezo

Shabiki wa soka kahukumiwa kwenda jela England

on

Baada ya kutenda kosa lisilokuwa la kiungwana kwa shabiki wa club ya Birmgham City Paul Mitchell ya kumshambulia staa wa Aston Villa Jack Grealish wakati wa mchezo wa Championship kati ya Birmgham City dhidi ya Aston Villa uliyomalizika kwa Aston Villa kushinda 1-0.

Paul Mitchell mwenye umri wa miaka 27 kwa kukiri hadharani kutenda kosa la kumshambulia Jack Grealish wakati wa mchezo huo kwa kuingia uwanjani, amehukumiwa kifungo cha miezi 14 jela, faini ya pound 35o pamoja na kufungiwa kwa miaka 10 kuingia uwanjani kuangalia mechi yoyote katika ardhi ya UK.

Kufuatia tukio hilo kujitokeza na tukio la shabiki mwingine kuonekana akiingia uwanjani wakati wa mchezo wa Arsenal dhidi ya Man United, chama cha soka England FA kimetangaza kuongeza ulinzi kwa wachezaji na waamuzi wakati wa michezo mbalimbali sambamba na kufanya kazi na taasisi nyingine binafsi ambazo zitasaidia kulinda usalama wa wachezaji.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments