Michezo

Jose Mourinho anatamani kurudi Chelsea sio Real Madrid

on

Baada ya kufukuzwa kazi na uongozi wa Man United kwa kocha wa kireno Jose Mourinho, mashabiki wengi wa soka wanatamani kujua mreno huyo ana mpango wa kwenda timu gani kuifundisha tena licha ya kuhusishwa na vilabu kadhaa ikiwemo club yake ya zamani ya Real Madrid.

Mourinho alipata nafasi ya kufanya mahojiano na beINSports na alipoulizwa kama ana mpango wa kurudi kufanya kazi katika club aliyowahi kufanya kazi awali alijibu kuwa ndio ni furaha na fahari kubwa kwake kurudi kama watakuwa wameona umuhimu wake na kumuhitaji kama ni Chelsea lakini kwa Real Madrid hapana.

“Kurudi timu ambayo nilikuwa awali sio tatizo kama wameniita tena kama naona ni wakati sahihi, kuna mfumo sahihi na malengo ya mbali hakuna shida kwa mimi kurudi katika club ambayo nimewahi kufanya kazi awali, nafikiri ni fahari kubwa wakati club uliyowahi kuifanyia kazi kukuita tena”>>> Jose Mourinho

“Lakini kwa sasa nina hamu ya kurudi Chelsea sio Real Madrid, hapana naipenda Hispania lakini sichagua timu kwa sababu ya nchi au hali ya hewa”>>> Jose Mourinho

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Jose Mourinho amewahi kufanya kazi na vilabu tofauti tofauti kwa nyakati tofauti ikiwemo Real Madrid na Chelsea, Chelsea amewahi kuifundisha katika vipindi viwili (2004-2007) na (2013-2015) wakati Real Madrid amewahi kuifundisha kwa miaka mitatu (2010-2013).

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments