AyoTV

Kocha Mwinyi Zahera na Makambo wa Yanga wakabidhiwa tuzo zao rasmi

on

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya BikoSports leo kupitia kwa afisa uhusiano wao Geof Lea imekabidhi tuzo kwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera na mshambuliaji wa timu hiyo Heritier Makambo ambao walikuwa wameshinda tuzo hizo.

Makambo na alifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi December 2018 wakati kocha Mwinyi Zahera alifanikiwa kushinda tuzo ya Kocha Bora wa mwezi December ikiwa ni mara ya tatu anashinda tuzo hiyo.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri shirikisho la soka Tanzania TFF liliingia mkataba wa udahmini na kampuni ya BikoSports kwa ajili ya kutoa zawadi na tuzo kwa washindi wa mchezaji bora wa mwezi na kocha bora sambamba na zawadi ya Tsh Milioni 1 kila mmoja kwa kipindi chote cha msimu wa Ligi Kuu 2018/2019 kilichosalia.

Msimamo wa Beno Kakolanya Yanga ndio huu, katuma tena barua

Soma na hizi

Tupia Comments