Club ya Huddersfield ya England leo imepata pigo katika Ligi Kuu England baada ya kujikuta inashuka daraja kutoka Ligi Kuu England hadi Champioship, Huddersfield leo ilicheza dhidi ya Crystal Palace ugenini na kujikuta wakipoteza mchezo kwa magoli 2-0 yaliofungwa na Milivojevic dakika ya 76 kwa penati na Van Aanholt dakika ya 88.
Kipigo hicho moja kwa moja kinaishusha Huddersfield kutoka Ligi Kuu England kwani hata wakishinda michezo yao yote sita iliyosalia, watakuwa na point 32, hivyo hawawezi kukaa nafasi ya 17 ambayo ni salama kwa kubakia Ligi Kuu kutokana na anayeimiliki hiyo nafasi Burnley tayari ana point 33.
Hivyo Huddersfield kwa sasa watakuwa wanacheza Ligi Kuu kukamilisha ratiba tu na kusubiri wenzao wengine wawili watakaoshuka nao Ligi Kuu msimu huu, Huddersfield wamekuwa timu ya pili England katika historia kuwahi kushuka Ligi Kuu ndani ya mwezi March kabla ya kuingia April yaani mapema zaidi.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars