Michezo

Mtoto wa Ronaldinho alivyokwepa kutumia ustaa wa baba yake

on

Imekuwa ni kawaida kwa watoto wa mastaa wa soka sehemu mbalimbali duniani kurithi kazi za baba zao, yaani kuendelea kukipiga katika soka kama ilivyo kwa baba zao, tofauti yao wao hupata urahisi wa kupata nafasi ya kuingia kwenye academy au team B za vilabu mbalimbali wakiaminika kuwa watarithi vipawa vya baba zao na kuwa mahiri.

Leo Jumapili ya April 7 2019 imeripotiwa taarifa ya kushangaza kidogo baada ya mtoto wa staa wa soka wa zamani wa Brazil na club ya FC Barcelona ya Hispania Ronaldinho, mwanae kusaini mkataba miaka mitano na club ya kwao Brazil inayojulikana kwa jina la Cruzeiro.

Kijana huyo anayejulikana kwa jina la Joao Mendes ana umri wa miaka 14 lakini hadi anasaini mkataba huo ndio club yake ikagundua kuwa ni mtoto wa Ronaldinho, mara zote amekuwa akifanya siri na kutotaka kupata mteremko kupitia jina la baba yake, Joao anacheza nafasi ya ushambuliaji na inaelezwa tayari kapewa nafasi ya kuingia katika kikosi cha kwanza katika club hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Brazil.

“Nina uhakika tunaweza kushinda Lubumbashi na kufuzu”- Kocha Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments