Habari za Mastaa

Rapa wa Marekani aliyeamua kuifuta instagram account yake kisa mapenzi

on

Rapa Travis Scott ameonekana kuonesha u-seriousness zaidi kwa mpenzi wake Kylie Jenner ili kumuonesha zaidi kuwa ana mpenda na hataki kumkwaza, Travis alikuwa katika tuhuma za kuhisiwa kuwa anafanya usaliti kutokana na kuonekana na meseji (DM Message) tofauti tofauti zilizomtia hofu Kylie Jenner .

Kylie Jenner katika instagram DM ya Travis Scott ambaye ni boyfriend wake amekutana na meseji ambazo zinashutumiwa kuwa za kumsaliti, ambapo rapa Travis Scott amekuwa akichati na wanawake tofauti tofauti, baada ya kuona Kylie Jenner  anaumia kwa kuhisi usaliti kufanyika Travis kafanya maamuzi mazito.

Rapa Travis Scott ameshindwa kujizuia na kuamua kumuonesha commitment zaidi girlfriend wake ambaye ni Kylie Jenner  kwa kuamua kujiondoa katika mtandao wa instagram, hiyo ikiwa ni njia ya kumthibitishia kuwa ameamua kukaa mbali  na vishawishi ambavyo vinamtia hofu Kyler.

MSAMI: “Kila ninapopanda kwenye steji, uwepo wake utakuwa pembeni yangu”

Soma na hizi

Tupia Comments