Club ya Nantes ya Ufaransa imeripotiwa kuanza kuidai club ya Cardiff City ada ya usajili wa mchezaji Emiliano Sala aliyejiunga na club hiyo siku chache kabla ya kupotea na ndege akiwa na rubani wake David Ibbotson ambapo wote wadahofiwa kupoteza maisha.
Nantes ambayo ilimuuza Emiliano Sala raia wa Argentina kwa dau la pound milioni 15 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 45 kwenda Cardiff City ya Wales, ila mchezaji huyo alirudi Nantes kuaga wachezaji wenzake baada ya kusaini mkataba wa kuichezea Cardiff.
January 21 akiwa njiani kuelekea Cardiff kuanza maisha mapya ya soka alipotea na ndege akiwa na rubani wake David Ibbotson ila mtandao wa mirror umeripoti kuwa tayari Nantes ikiwa bado mwili wa Emiliano Sala na rubani wake David Ibbotson haijapatika wameanza kudai malipo ya usajili wa mchezaji huyo.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF