Michezo

Ngorongoro Heroes wametoboa hadi fainali CECAFA U-20

on

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania wenye umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes, leo wameendeleza ubabe wao dhidi ya Sudan katika mchezo wa nusu fainali wa CECAFA U-20.

Ngorongoro Heroes leo imefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuifunga Sudan 2-1, magoli ya Tanzania yakifungwa na Patrick Mwenda dakika ya 39 na Kelvin John dakika ya 45.

Sudan wamemaliza mchezo wakiishia goli moja lililofungwa dakika ya 52 na Mohammed Abbas, sasa Tanzania U-20 itajua itacheza na nani fainali baada ya kujua mshindi wa nusu fainali ya pili.

Soma na hizi

Tupia Comments