Habari za Mastaa

Unajua ngoma ambayo Rais Obama kaisikiliza zaidi mwaka 2015? Ni hii ya Hiphop.. (+Audio)

on

Amini usiamini mtu wangu, Rais wa Marekani, Barack Obama ni miongoni wa viongozi wachache wa dunia wenye upendo mkubwa sana na muziki wa kizazi kipya na miondoko anayoikubali zaidi ni fleva za HipHop!

Nimekutana na stori ya Rais Obama inayoweka headlines za kila aina kwenye mitandao ya Marekani… je unajua  ya kuwa Rais Obama anasikiliza sana muziki wa HipHop na kwa mwaka huu wa 2015 best ama favorite song wa Rais huyo wa Marekani ni..? Ipokee hii.

OBAMA4

Rais wa Marekani, Barack Obama.

Nimekutana na interview aliyofanya Rais Barack Obama na jarida la PEOPLE Magazine, na humo Obama aliweka wazi kuwa yeye ni shabiki mkubwa sana wa rapper Kendrick Lamar na kwa mwaka huu wa 2015 wimbo wake wa ‘How Much a Dollar Cost’ ndio wimbo unaochezwa zaidi kwenye playlist yake.

OBAMA1

Barack Obama & Kendrick Lamar.

Kwenye mazungumzo na jarida hilo Rais Obama alisisitiza kuwa wimbo huo umebeba ujumbe mzito sana na hajawahi kuchoka kuusikiliza na kila anapokuwa free basi hiyo ndio ngoma anayopenda kuisikiliza zaidi, huku mke wake Michelle Obama anaukubali sana wimbo wa Bruno Mars  ‘Uptown Funk’ na kusema huo ndio wimbo wa mwaka kwa First Lady huyo.

OBAMA2

Rais Barack Obama & First Lady Michelle Obama.

Licha ya hayo kwenye playlist ya Rais Barack Obama majina ya mastaa hawa ni lazima ukutane nayo; Beyonce Knowles, Justin Tmberlake, Frank Ocean, Erykah Badu, Mary J Blige na Mos Def.

Usikilize wimbo huo wa Kendrick Lamar (How Much A Dollar Cost) hapa chini:

https://youtu.be/CFqFeS_ivZQ

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

 

Soma na hizi

Tupia Comments