Mix

Obama kaamua kutimiza ahadi ya kutembelea kwao KENYA?

on

Barack Obama

Kila mtu anafahamu kwamba marehemu baba mzazi wa Rais wa Marekani Barrack Obama ana asili ya Kenya, lakini mara nyingi amekuwa akiulizwa kwamba kwa nini tangu amekuwa Rais wa Marekani hajawahi kutembelea kwenye nchi hiyo.

Hilo swali kawahi kuulizwa zaidi ya mara mbili, lakini alipokuwa South Africa mwaka 2013 alijibu kwamba kwa sababu hajamaliza uongozi wake, basi tusubiri hiyo safari ya kutembelea Kenya huenda ikawepo wakati wowote.

Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani leo imetangaza kuwa Rais Obama atarajiwa kwenda Kenya mwezi July 2015 ambapo atakuwa akihudhuria Mkutano mkubwa wa kibiashara na ujasiriamali utakaofanyika Nairobi.

Labda kitu ambacho Wakenya wengi hawakukipenda ni ishu ya Rais huyo kutembelea nchi nyingine kama Tanzania, Senegal na Afrika Kusini lakini hakufika nyumbani kwao.

Hii ilikuwa Obama alipotembelea Dakar, Senegal 2013.

Hii ilikuwa Obama alipotembelea Dakar, Senegal 2013.

Mara ya mwisho Obama kufika Kenya ilikuwa mwaka 2006 ambapo wakati huo alikuwa bado Seneta wa Illinois, Marekani.

Ikulu ya Marekani wamesema wataendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu safari hiyo.

Obama II

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments