Naibu Katibu Mkuu wizara ya maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba akiwa kwenye mkutano wa wizara za kisekta jijini Dodoma unaolenga kuokoa shoroba za wanyapori zilizovamiwa na wananchi amesema kuonekana kwa wanyamapori kwenye makazi ya watu ni kutokana na wananchi kuvamia kwenye mapito ya Wanyama hao (shoroba).
Kamishna Wakulyamba ameongeza kuwa changamoto ya kuvamiwa kwa maeneo ya Shoroba za Wanyamapori ni suala linalogusa Wizara mbalimbali za Kisekta ikiwemo Ofisi ya Rais TAMISEMI,Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya Makazi,Kilimo,Ujenzi,Maji na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Kwa upande wake Mtafiti Mkuu Wanyamapori kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Dkt. Hamza Kija amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori iliainisha takribani Shoroba 61 nchini ambapo kati ya hizo zikachaguliwa shoroba 20 za kipaumbele kutokana na umuhimu wake kiikolojia,kiuchumi, kisiasa, na umuhimu katika shughuli za utalii.