Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Kocha Ndairagije kamkabidhi kitambaa cha unahodha John Bocco

on

Kuelekea mchezo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kuwania kufuzu kucheza michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani CHAN dhidi ya Kenya Jumapili ya July 28 2019.

Kaimu Kocha mkuu wa Taifa Stars Etienne Ndairagije amemtangaza nahodha wa Simba SC John Raphael Bocco kuwa nahodha wa kikosi hicho cha wachezaji wa ndani na wasaidizi wake ni Juma Kaseja, Kelvin Yondani na Erasto Nyoni.

John Bocco

Taifa Stars italazimika kupata matokeo chanya dhidi ya Kenya katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini na ikifanikiwa kuitoa Kenya itacheza dhidi ya Sudan na kufuzu CHAN kama itapata matokeo mazuri.

Soma na hizi

Tupia Comments