Michezo

June 8 ndio itafahamika Pamba, Geita au Kagera na Mwadui 2019/2020

on

Pamoja na kuwa Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2018/2019 imemalizika kwa Simba SC kuibuka na Ubingwa, vita bado ipo kwa timu za Ligi daraja la kwanza zinazowania kupanda Pamba FC ya Mwanza na Geita Gold pamoja na timu za Ligi Kuu Kagera Sugar na Mwadui FC zinazowania kubaki Ligi Kuu.

Leo timu za Geita ilikuwa nyumbani kucheza dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa kwanza wa Play Off ambao ulimalizika kwa sare 0-0, wakati Pamba FC nao wakiwa Nyamagana Mwanza kucheza dhidi ya Kagera Sugar mchezo ambao ulimalizika kwa sare 0-0.

Matokeo hayo sasa yanafanya nafasi ya timu zote kupanda Ligi Kuu kuwa wazi hadi June 8 watakapocheza game za marudiano, kwani timu itakayoshinda ndio itapanda kucheza Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2019/2020, hivyo Pamba na Geita wana kazi game zao za marudiano ugenini.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments