Afisa Habari wa zamani wa Yanga Jerry Muro amedai kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF linawagawa mashabiki wa mchezo huo nchini ili liwatawale.
Muro amesema kuwa kitendo cha TFF kumfungia yeye pamoja na Afisa Habari wa Simba Haji S. Manara ni kwa sababu Shirikisho hilo linajaribu kuwagawa wapenda mpira Tanzania ili liwatawale vizuri.
Akizungumza kwenye Clouds 360 ya Clouds TV April 29, 2017 Muro ameweka wazi kuwa atarudi katika nafasi yake katika klabu ya Yanga mara tu atakapomaliza adhabu yake, akisema: “Yah! Mimi ni mwanachama wa Yanga tangu nikiwa mdogo. Nilipokuwa Yanga, nilikuwa nafanya kazi zangu kama kawaida na Yanga siondoki. Akili ndogo inapokuambia kaa pembeni, unakaa pembeni kwa sababu akili kubwa haiwezi kupambana na akili ndogo.
“Nilipofungiwa mimi, niliwaambiwa mashabiki tupambane nisifungiwe hawa watu wanatugawanya. Leo wananifungia mimi, kesho watamfungia Manara. Marana amefungiwa, wametugawanya na wanatutawala. Ndio maana nasema, tusikubali akili ndogo kuongoza akili kubwa.
“Unaponiondoa mimi na Haji kwenye mpira, mbadala ni nani? Sisi tumeingia kwenye mpira, mpira ulikuwa umepooza. Tumepandisha morari kwenye mpira, tumeinua hamasa. Zile nafasi zipo kwa ajili yetu ndio maana tangu nimeondoka Yanga, nani amevaa viatu vyangu?” – Jerry Muro.
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full story nimekuwekea
VIDEO: Adhabu aliyopewa Haji Manara wa Simba na kamati ya nidhamu ya TFF