Michezo

Breaking News inamuhusu Okwi ndani ya Denmark kwenye uthibitisho wa picha kabisa..

on

Siku kadhaa baada ya kumaliza majaribio ya wiki mbili katika klabu ya Sonderjyske inayoshiriki katika ligi kuu ya Denmark, mshambuliaji Emmanuel Okwi amefaulu majaribio hayo. 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ya Denmark, mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa na Simba msimu uliopita akitokea Yanga amejiunga rasmi na timu hiyo baada ya kufuzu majaribio yake.

Okwi amesaini mkataba wa miaka 5 wa kuitumikia klabu hiyo na leo ametambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari akikibidhiwa jezi namba 25.
 Mpaka sasa haijawekwa wazi ni kiasi gani klabu ya Simba imelipwa kuumuza Okwi ambaye miaka kadhaa nyuma walimuuza kwa Dola 300,000 kwenda klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia kabla hajarejea Tanzani kuitumikia Yanga.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments