Michezo

Emmanuel Okwi azungumza kuhusu taarifa za kuondoka Yanga, hiki ndicho alichosema

on

OKWISiku kadhaa baada ya kutoka taarifa kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda anayekipiga klabu bingwa ya Tanzania bara Yanga, Emmanuel Okwi amegoma kuendelea kuichezea timu hiyo kutokana na kuidai timu hiyo, hatimaye leo hii kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook Okwi amevunja ukimya na kuzungumzia suala hilo.

Hiki ndicho alichoandika leo

OKWI copy

 

Kwa mujibu wa Okwi sio kweli kwamba ameondoka Yanga, bali amepata majeraha ya goti yanayomfanya asiwepo kwenye kikosi cha Yanga. Amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa imani waliyonayo juu yake na kuahidi kurudi dimbani kuitumikia klabu hiyo atakapopona.

Tupia Comments