Mix

Hii rekodi ya mpangaji kukaa muda mrefu kwenye nyumba moja ndio kwanza naisikia toka Kenya.. (VIDEO)

on

KEYS_2603460b
Nyumba nyingi za kupanga zimekuwa na changamoto zake!.. Umewahi kukaa kwa muda gani kwenye nyumba za kupanga bila kuhama au umeshahama nyumba ngapi mpaka sasa?

Hii sio mbali sana, inatokea mtaa wa Old Ngara, Kenya ambako kuna mzee mmoja ambae ameishi kwenye nyumba kwa muda mrefu, hii rekodi sikuwahi kuisikia kwingine.

NYUMBA

Mzee huyo Adam Mamuji amesema ameishi kwenye nyumba hiyo tangu mwaka 1944 kabla nchi hiyo haijapata uhuru, wakati huo alikuwa akiishi na wazazi wake ambao walifariki.. kipindi hicho kodi ilikuwa shilingi 45 za Kenya.

Mzee Adam amesema mwaka 1948 kodi ilipanda na kufikia shilingi 140, lakini kwa sasa wanalipa shilingi elfu 10 za Kenya.. amesema hawezi kutafuta nyumba nyingine tena kwa sababu ameishi kwa muda mrefu kwenye nyumba hiyo ameiomba Serikali imuuzie.

Nimeamini hakuna watu watunzaji wa vitu kama wazee, huyu mzee ametoa mpaka risiti ya Kodi ya nyumba aliyolipia miaka ya 1940 !!

Hii story yote iko kwenye video hapa ambayo iliripotiwa na kituo cha K24 Kenya..

millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, movies, magazeti, video mpya na nyingine kubwa….  unaweza kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments