Top Stories

Ole Sabaya, IGP Sirro watajwa kesi ya Mbowe Mahakamani Kisutu “Tumeomba waletwe”

on

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Wenzake wameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwamba watamtumia aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro kama Mashahidi wao wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu “Mahakama ya Mafisadi”.

Hayo yamebainishwa na Wakili wa Mbowe na Wenzake, Peter Kibatala baada ya kesi hiyo kuletwa chini ya hati ya dharura leo huku washtakiwa hao wakisomewa mashtaka upya na kufikia mashtaka saba ikiwemo la kutaka kumdhuru Sabaya.

Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba anayesikiliza kesi hiyo amesema kwamba mchakato wa kesi hiyo kwenda Mahakama ya Mafisadi umekamilika.

ULINZI: MBOWE NA WENZAKE WARUDISHWA MAHAKAMANI KISUTU, KESI YA UGAIDI NA UHUJUMU UCHUMI

 

Soma na hizi

Tupia Comments