Hali ya afya ya mshambuliaji wa Olympiakos Michael Olaitan aliyelazwa katika hospitali moja nchini Ugiriki inasemekana kuwa nzuri.
Mchezaji huyo alikimbizwa hospitalini baada ya kuzirai wakati wa kipindi cha kwanza cha pambano dhidi ya watani wa jadi Panathinaikos ambapo walifungwa 3-0 mjini Athens.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Nigeria huyo alikuwa akikimbia uwanjani alipoanguka.
Hapo awali meneja wa Panathinaikos Yannis Anastasiou, alianguka chini baada ya kuvurumishiwa kitu kutoka upande wa mashabiki.
Olaitan mwenye umri wa miaka 21 na ambae aliisaidia Olympiakos kuishinda Manchester United 2-0 February 25 alipata fahamu kabla ya kupelekwa hospitali kwa ukaguzi zaidi.
Hali yake iliarifiwa kuwa nzuri jioni ya Jumapili.
Alipozirai timu hizo zilikua hazijafungana, lakini Olympiakos ambao ndio wanaoongoza msimamo wa ligi kuu walifungwa bao kabla mapumziko na kuongeza mengine mawili kabla ya kipenga cha mwisho.
Licha ya kushindwa kwa mara ya kwanza msimu huu, Olympiakos wanacheza Old Trafford kwa mchezo wa marudiano ya kombe la klabu bingwa ya Ulaya.
Wanaongoza kwa pointi 19 Panathinaikos wanashikilia nafasi ya nne ikiwa pointi tano nyuma