Habari za Mastaa

Ommy Dimpoz kapewa mualiko na NBA kuhudhuria kwenye hili

on

Masanii wa muziki wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz amepata maualiko rasmi wa kuhudhuria michezo ya NBA All-Star ambayo itafanyika mjini Chicago Marekani kuanzia Februari 14 hadi 16 mwaka huu.

Ommy Dimpoz anakuja ni miongoni mwa Mastaa watatu kutokea  Afrika waliopewa mwaliko huo, hao wengine ni Sho Madjozi wa Afrika Kusini na Jidenna mwenye asili ya  Nigeria na Marekani.

Mualiko huo umetolewa na Chama cha Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA), kupitia NBA Africa ambao wamemgharamia kila kitu ikiwemo Usafiri wa ndege kwenda Marekani, usafiri wa ndani na gharama za kuishi.

Hata hivyo Ommy Dimpoz ameshare picha Kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa kwenye  Ndege na Seven Mosha ambaye amekuwa naye karibu Kwenye usimamizi wa baadhi ya kazi zake.

Soma na hizi

Tupia Comments