Habari za Mastaa

Marioo aeleza Nandy alivyomuwekea pozi siku ya kwanza, alivyosota Gereji baada ya kuacha Shule

on

Jina lake la passport ni Omari lakini la BASATA ni Marioo, Mkali alieandika ngoma kali kama ‘nabembea’ ya Ditto na ‘wasikudanganye’ ya Nandy na sasa yeye mwenyewe yuko kwenye game, sauti yake inasikika sana kwenye TOP 10 kwenye ngoma ya ‘chibonge’ na ‘inatosha’.

Unafahamu Marioo amefikaje alipo? kama hukufahamu ni kwamba aliishia Form One ambapo baada ya kushindwa kuendelea na Shule ilibidi arudi nyumbani na kama ilivyo desturi ya Jamii yake alilazimishwa kwenda kufanya kazi gereji, akasota kupiga kazi huko mpaka baada akaja kutoka kimuziki.

Marioo anasema moja ya Watu ambao hawakumuamini kabisa kwenye kuwaandikia nyimbo ni Nandy ambae anasema alimuwekea pozi siku ya kwanza, wakati huo ukubwa wa jina la Marioo haukuwa kama huu wa sasa, ni wachache walikua wanamfahamu na hata Nandy ndio ilikua mara ya kwanza wanakutana, stori nzima ilikuaje? maisha yake ya msoto? bonyeza play hapa chini kumtazama Marioo mwanzo mwisho.

NANDY EXCLUSIVE: “RUGE ALINICHUMBIA, NDOA INGEFUNGWA MARCH”

ROSA REE ASIMULIA MAISHA YAKE KWA MACHUNGU “ILIBIDI MAMA AKAOMBE MSAADA KANISANI”

Soma na hizi

Tupia Comments