Wimbo wa Bob Marley “One Love” uliotoka mwaka 1965 umeshinda tuzo za Grammy 2025 kama “Best Reggae Album” akiwashinda wanamuziki wengine kama Collie Buddz’s “Take It Easy” Shenseea’s “Never Gets Late Here” Vybz Kartel’s “Party With Me” pamoja na The Wailers “Evolution”.
Bob Marley ni mwanamuziki kutoka Jamaica aliyefariki 1981 mei akiacha alama kubwa katika muziki wa Reggae
Albamu hiyo yenye nyimbo 10 ina nyimbo kutoka kwa wajukuu wa Bob Marley Skip Marley, mtoto wa binti Cedella na Mystic Marley, binti wa mtoto wa kiume, Stephen;Shenseea; Kacey Musgraves, mshindi wa Wimbo Bora wa Nchi katika tuzo za mwaka huu; Daniel Caesar, Wizkid, Jessie Reyez, Leon Bridges na Farruko.
Albamu hiyo ni tofauti na wimbo wa wasifu wa Bob Marley:One Love, ambao ulitolewa rasmi Februari 14 mwaka jana.