Habari za Mastaa

Wizkid ameipa heshima hii One Dance ya Drake

on

Kismart cha star wa single ya Baba Nla, Ayodeji Ibrahim Balogun a.k.a Wizkid ambaye alipata nafasi kuperform kupitia Fiesta ya kwanza Jijini mwanza, kinazidi kuiweka Afrika kwenye ramani nzuri ya muziki kwa mara nyingine. 

Wizkid anaingia kwenye headlines za kimataifa baada ya single aliyoshirikishwa na rapa kutoka YMCMB Drake ya One Dance kuongoza katika list ya nyimbo zinazouzwa zaidi duniani kwa mwaka 2016 huku ikiishusha single ya Justin Bieber iliyokua ikiongoza kipindi cha nyuma. One Dance imetajwa kama “World’s best-selling Single of 2016!

Single ya Justin Bieber, Love Yourself’ iliweka rekodi hiyo mpaka kufikia mwezi August 2016.

Sasa mpaka kufikia mwanzoni mwa mwezi September 2016, One Dance ya Drake na Wizkid inaongoza kwenye list hiyo. ‘Love Yourself’ imeshuka mpaka  No.2 huku mzigo wa ‘Can’t Stop This Feeling’ wa Justin Timberlake ikiwa No.3. na ‘Stressed Out’ ya twenty one pilots ikishika No.4!

ULIMISS SHOW YA WIZKID KWENYE FIESTA MWANZA? ITAZAME HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments